MAELEZO YA MFUMOByteq Biashara ni nini?
Ni mfumo wa usimamizi wa biashara unaotumika kupitia simu, tablet au computer. Unamruhusu mmiliki kuweka na kuona taarifa za biashara yake katika sehemu moja.
Badala ya kutegemea daftari pekee, unaweza kuona mauzo, bidhaa zilizopo, matumizi, madeni na taarifa nyingine muhimu kwa urahisi.
SABABU YA MFUMOKwa nini mfumo huu upo?
Biashara nyingi zina taarifa muhimu kwenye madaftari tofauti, simu au kumbukumbu za watu. Hali hii inaweza kufanya taarifa kuwa ngumu kufuatilia.
Byteq Biashara inaleta taarifa hizo pamoja ili mmiliki aelewe biashara yake vizuri na afanye maamuzi akiwa na taarifa.